MAGONJWA YA VIUNGO NA MIFUPA.
UGONJWA WA MIFUPA NA MAUNGIO
MAGONJWA MIFUPA NA MAUNGIO
UTANGULIZI
Maumivu ya joint ni tatizo l inalosumbua watu wengi kwa sasa kutokana na mabadiliko ya mitindo ya Maisha. Umri mkubwa ni moja ya sababu inayopelekea kutokea kwa tatizo, ambapo tishu za mwili zinakuwa kavu na kupoteza uwezo wa kuvutika. Watu wengi wanfikiri kwamba kufanya mazoezi ni hatari kwa afya ya joints lakini ukweli ni kwamba ili kuepuka magonjwa ya joints mazoezi ni lazima katika akuongeza ufanisi wa viungo pia.
Nina uhakika kuwa umewaona akina mama wenye umri mkubwa na miili mikubwa wanavyopata shida kutembea huku wakiinama toka upande mmoja hadi mwingine kila wakipiga hatua au shida wanayopata pale inapowabidi kupanda ngazi au kuchuchumaa. Maneno kama “ugonjwa wa kuumwa joints, nina tatizo la joints, maumivu ya joints” na maumivu ya mifupa umeyasikia mara nyingi. Tatizo hili haswa hujulikana kama ugonjwa wa arthritis.
UGONJWA WA ARTHRITIS NI NINI?
Arthritis ni ugonjwa unaotokana na namna yo yote ya hitilafu katika maungio ya mifupa ya binadamu ambao husababisha maumivu na pengine kuvimba katika sehemu moja au zaidi ya maungio hayo. Neno arthritis halilengi ugonjwa mmoja bali jamii ya magonjwa ambayo kwa ujumla yapo zaidi ya 100. Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo moja.
CHANZO CHA ARTHRITIS NI NINI?
Kusudi kuelewa chanzo cha ugonjwa huu, hebu kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana. Fikiria goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana:
Ligaments: Ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja. Hii ni kama utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje, ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.
Cartilage: Huu ni utando unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja. Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.
Capsule: Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote. Ndani ya mfuko huu wa capsule kuna synovial fluid ambayo huzalishwa na synovial membrane. Synovial fluid ni ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.
Ugonjwa wa arthritis unasababishwa na hitilafu yoyote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa. Inaweza kuwa cartilage inalika, upungufu wa synovial fluid, maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.
AINA ZA UGONJWA WA JOINTS-ARTHRITIS
Kama nilivyoeleza hapo juu, kuna aina zaidi ya 100 za ugonjwa huu wa joints au arthritis, tutatazama aina kama nne hivi za ugonjwa huu, tukielezea chanzo cha kila aina.
a) OSTEOARTHRITIS: Hii ni aina ya arthritis inayosumbua watu wengi zaidi kuliko aina nyingine zote. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa. Osteoarthritis hutokea pale cartilage inapopoteza uwezo wake wa kubonyea na kuwa ngumu hivyo kuharibika haraka. Cartilage ni kiungo cha kuhimili migandamizo ya ghafla (shock absorber). Cartilage hii inapopoteza ubora wake, tendons na ligaments huvutika na kusababisha maumivu. Hali ya uharibifu huu wa cartilage ikiendelea, mwishowe mifupa
huanza kusuguana moja kwa moja na ndipo mgonjwa atakapoanza kupata maumivu makali sana.
ATHARI ZA UGONJWA
Athari za ugonjwa huanza taratibu na kuongezeka na muda. Kutaanza kutokea maumivu kwenye joint baada ya kufanya shuguli fulani au baada ya mapumziko ya muda mrefu. Joints zitakaza, hasa mapema asubuhi unapotaka kuanza shughuli zako za kawaida. Siku zinavyosogea ndivyo utakavyoona ni vigumu zaidi kukitumia kiungo chako. Mara nyingine utaona uvimbe kwenye joint. Osteoarthritis hushambulia zaidi nyonga, mikono, magoti na uti wa mgongo
b) RHEUMATOID ARTHRITIS: Ugonjwa huu hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili kwa bahati mbaya kuanza kushambulia viungo vya mwili ikiwa ni pamoja na synovial membrane (synovium) na kusababisha uvimbe na maumivu. Hali hii isipodhibitiwa itafanya mtu asitembee kabsa hata kujihusisha na kazi za mikono,, Sasa njoo *bf SUMA upateee suluhuu ndani y siku c
hachee* saana _.0675601966_
No comments