UGONJWA WA PID:
*UGONJWA WA PID* (Pelvic Inflammatory Disease)
au Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa
Mwanamke.
Magonjwa ya zinaa ndio sababu kuu ya
wanawake kupata maambukizi katika mfumo wa
uzazi yani (PID). Mwanamke 1 kati ya wanawake 8 walipota PID katika wakati wowote ndani ya maisha yao hupata tabu kushika mimba
*(PID) NI NINI?*
PID ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa
mwanamke na mara nyingi husababishwa na
magonjwa ya zinaa kama gonorrhea na
chlamydia ila kuna aina ya maambukizi mbali na
magonjwa ya zinaa yanaweza kusababisha
maambukizi ya PID.
*JE! MWANAMKE HUAMBUKIZWAJE PID?*
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza
kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na:
- Kama una ugonjwa wa zinaa na haijatibiwa
- Kufanya ngono zembe isiyo salama (yani kulala
na wanaume tafauti tafauti)
- Kuwa na mpenzi ambaye ana wanawake wengi
nnje
- Kama umekuwepo na historia ya PID hapo
nyuma
- Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara
baada ya kujifungua (au postpartum period)
- Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya
kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post
abortion) au mara baada ya mimba kutoka
(miscarriage)
- Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa
uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa
mpango
- Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya
PID
- Kutumia (Vaginal Dauche)
*UTAJUAJE UKO NA (PID)?*
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID.
Miongoni mwa dalili hizi ni:
- Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa
maeneo ya chini ya kitovu
- Kupata maumivu ya mgongo
- Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za
siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kupata maumivu au kutokwa na damu wakati
wa tendo la ndoa
- Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
- Kupata homa
- Kupata damu innje ya siku zako zako za-
kawaida kupata damu ya hedhi
- Wakati fulani kuhisi kichefuchefu kama
mwanamke mja mzito na kutapika
*VIPIMO VYA PID*
Hakuna vipimo maalum kudhibitisha mwanamke
ameathirika ila Dactari hujua mwanamke
ameathirika baada ya kuchukua historia ya
muhusika na kufanya vipimo vingine kama:
- Kuchunguza mkojo ili kufahamu kama mgonjwa
ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa
mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au
mwenye uwezo wa kubeba mimba
- Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili
kutambua aina za vimelea vinavyomletea
mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza
kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua
aina nyingine za vimelea viletavyo uambukizi huo.
- Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza jinsi aina
mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na
uambukizi huo au kama kuna mwingiliano na
magonjwa mengine yaliyojificha. Kipimo hiki kwa
kitaalamu huitwa (Full Blood Picture).
- Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi
na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za
vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki
huitwa (Cervical culture)
- Aidha ni muhimu pia kufanya vipimo vingine kwa
ajili ya utambuzi wa magonjwa yaambukizwayo
kwa njia ya kujamiiana, kama vile virusi vya
ukimwi na kisonono.
- Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya
nyonga ili kuangalia kama kuna athari yeyote
katika mfumo wake wa uzazi.
*JE PID INAWEZA KUTIBIWA?*
Jibu ni ndio kama itagunduliwa mapema inaweza
kutibiwa na ikaisha, ila ieleweke kama tayari
ilikuwa imeharibu njia za uzazi uharibifu ule
haiwezi kurekebishwa. Kila mara ukichelewesha
kutibu PID ndivyo itaharibu mfumo wako wote wa
uzazi sasa ni muhimu ukiona mojawapo wa dalili
nilizozitaja utembelee daktari ili upate tiba. Hata
kama utatibiwa na zile dalili zikapotea hakikisha
kila mara unashauriana na daktari wako na
ukipata mume mwingine ni muhimu umueleze ili
mpate matibabu msi-ambukizane mara kwa
mara. Ijulikane kama ulikuwa na PID awali
inaweza kurudi mara kwa mara.
*MATIBABU*
Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa
ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya
antibayotiki huweza kutumika kwa ajili ya kuua
vimelea vya ugonjwa .
Ieleweke pia mara nyingi ugonjwa hujirudia mara
kwa mara kama mwanamke atapewa tiba na
mume asitibiwe. Na kama maambukizi imekuwa
sugu inabidi muathiriwa amueleze daktari ili
apate kutumia anti-biotics kwa mda mrefu kuliko
kawaida. Lakini muhimu sana mwanaume apewe
dawa wakati mwanamke anatibiwa. Ikiwa
mwanamke peke yake atapata tiba pindi atakapo
lala na mwanaume yule yule maambukizi
yatarejelea.
*MADHARA YAKUTO-FWATA MATIBABU*
- Maumivu ya mfuko wa uzazi wakudumu
- Utapata ugumu wa kushika mimba
- Ectopic pregnancy (mtoto kuwa innje ya mfuko
wa uzazi)
- Kuziba kwa njia ya uzazi
*JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI*
Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika
mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na:
- Njia hakiki ya kujizuia na maambukizi haya ni
kuwacha ngono zembe na kufanya ngono salama
- Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili
za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu
unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za
magonjwa ya zinaa au anatembea na wanawake
wengine
- Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya
mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya
maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa
njia ya ngono (STI) khususan ugonjwa wa
chlamydia ufanyie vipimo kila mwaka mara 1
- Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua,
mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili
kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga
vema.
Ahsante.
No comments